Taasisi ya PDS Zanzibar inawatangazia vijana wote hasa kutoka Mkoa wa Kusini Unguja kushiriki katika Mafunzo ya Siku mbili yenye lengo la kujenga uwezo katika masuala ya Biashara zenye tija na kukuza ujuzi na uwelewa wa namna gani Biashara hizo zinaweza kuwa chachu ya kufikia usawa wa kijinsia, kulinda Mazingira, kutatua mabadiliko ya tabia ya Nchi na kubadilisha jamii yako.
PROGRAM
Karibu Herstart: Innovate the future ni mradi wa Shirika la Youth Challenge International unaolenga kusuma maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii kwa wanawake na jamii zao Nchini Ghana, Tanzania, na Uganda.
Mradi unalengo la;
- Kujenga uwezo wa kiuongozi, kujitambua na ujasiri.
- Kuongeza uelewa wa uwezo wa mabadiliko ya kijamii kupitia Biashara inayohusisha fursa za uchumi wa kijani (Green Economy).
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe mwanamke kunzia umri wa miaka 18-35
- Awe na uwezo wa kusoma na kuandika
- Awe hajadahiliwa katika Mafunzo ya shule
- Awe na uwezo wa kuhudhuria siku 2-3 za mafunzo
- Awe anapenda ujasiri amali, kujiajiri au kuleta mabadiliko chanya katika Jamii yake
- Awe anapatikana Zanzibar
- Awe tayari kujigharamia usafri wa kwenda na kurud katika Mafunzo
SIKU NA WAKATI
Tutakujulisha baada ya kukuchagua kushiriki katika Mafunzo.
SEHEMU?
Mafunzo yatafanyika katika Ofisi kuu ya PDS Tunguu Kibele, Zanzibar.
KWA MAELEZO ZAIDI
Kufanya maombi, Unatakiwa uje Ofisi ya PDS kujaza Fomu ama unaweza kuchukua fomu katika Ofisi ya Vijana Wilaya ya Kati Unguja
Au uende moja kwa moja Wizara ya Habari kwenye Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar.