Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya PDS Zanzibar Charitable Organization anakaribisha maombi ya nafasi tatu (3) za kazi za kujitolea (local volunteers) katika skuli ya PDS iliopo Tunguu.
SIFA ZA MUOMBAJI
Mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI), Awe amehitimu cheti/stashahada katika moja ya fani zifuatazo; Maendeleo ya jamii, uwalimu, lishe ama afya kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
POSHO
Nafasi zote tatu zitakuwa na posho ya usafiri ambalo litatolewa kila mwisho wa mwezi.
MAELEZO YA ZIADA
Fomu hii ni kwa ajili tu ya kufahamu watu wenye hamu (interest) ya kuomba nafasi hizi, baada ya kupokea taarifa fupi kwa waombaji kupitia fomu hii, tutawatumia email za maelekezo ya kina juu ya namna gani kukamilisha maombi haya
Wahi kuanza kufanya maombi mapema, kwani nafasi ni chache na watu wanahitajika haraka.
IMETOLEWA NA:
Ramla Ramadhan Ameir
Katibu wa Mkurugenzi mtendaji
PDS Zanzibar
Mob. 0688 411345/0628802252